Uncategorised
- Details

“Isaya 9:2 “Watu wale waliokwenda katika giza wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza.”
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mhashamu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewataka vijana wa KKKT-DKMs kugeuza mitandao ya kijamii kuwa fursa kwa kuitumia vema kupata maarifa na uzoefu katika nyanja mbalimbali na kujiepusha na matumizi yasiyofaa.
- Details

Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju amewashukuru na kuwapongeza wachungaji wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa kazi nzuri wanazozifanya katika Sharika zao ikiwemo mikutano na semina mbalimbali za neno la Mungu walizozifanya mwaka huu wa 2022.
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt. Solomon Jacobo Massangwa amemshukuru na kumpongeza Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, kwa kukubali kuwapokea washarika wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania waliohama kutoka KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati Usharika wa Enndulen-Ngorongoro na kuhamia KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki katika Jimbo la Tambarare Usharika wa Handeni Mtaa wa Msomera.
Page 63 of 124

