Tarehe 21/09/2023 akiwa nchini  Ujerumani Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alialikwa kwenye kiwanda cha kutengeneza makontena na stoo maalum zinazozuia moto, kiwanda hiki  kinasimamiwa na kampuni ya  DENIOS. Hapa Baba Askofu alikutana  na baadhi ya marafiki walioonyesha moyo wa kujitolea kufadhili mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Makose kilichoko kwenye Usharika wa Mwangoi. Kutoka kulia ni Bw. Ernst-Ludwig Homann (anayesimamia mawasiliano kati ya Usaharika wa Mwangoi na Usharika rafiki wa Bergkirchen - Ujerumani), Bw. Helmut Dennig (Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kampuni ya DENIOS) na Askofu Dkt. Mbilu. Mradi huu ambao utatekelezwa na kusimamiwa na Usharika rafiki wa Bergkirchen ni miongoni mwa miradi kadhaa ya maji iliyowekwa kwenye eneo la Usharika wa Mwangoi wa KKKT - Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Msaidizi wa Askofu, KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Michael Mlondakweli Kanju amewashukuru Washarika wa Usharika wa Mgwashi na wanadayosisi kwa namna wanavyo endelea kujitoa kwa hali na mali kuchangia deni linaloikabili Dayosisi.

Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akiwa na Cardinal Kurt Koch, ambaye alipata nafasi ya kufika kwenye Mkutano Mkuu wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (LWF), huyu ni  kiongozi wa ngazi ya juu ndani ya  Kanisa Katoliki. Cardinal  Koch,ndiye anayehusika na maswala ya kuimarisha na kuendeleza Umoja wa Kikristo katika ofisi ya Papa, Vatican ( Prefect of the Vatican Dicastery for Promoting Christian Unity).

Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  Mch. Michael Mlondakweli Kanju amewaasa Washarika wa Kabuku, Jimbo teule la Magharibi na Wakristo kwa ujumla  kuchora alama ya msalaba mioyoni mwao na kumkaribisha Yesu katika maisha yao na waache kuangalia ukubwa wa tatizo na badala yake wamwangalie Yesu. Pia amesema wakianguka na kushindwa wasizame kwenye dhambi bali waamke na kuutafuta uso wa Bwana.