Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu tarehe 01/11/2023 ameongoza  Ibada ya mazishi ya marehemu Mch. Msataafu Mzee Mpewa Lazaro Ruwa iliyofanyika katika Jimbo la Pwani Usharika wa Makorora Tanga.

Marehemu Mzee Ruwa aliitwa mbinguni tarehe 28/10/2023  akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo na mwili wake umepumzishwa tarehe 01/11/2023 katika makaburi yaliyopo katika eneo la Gofu Tanga.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,ni mmoja wa wageni walioalikwa kwenye  hafla ya Chakula cha Jioni iliyoandaliwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania . Hafla hii ilifanyikia tarehe 31/10/2023 katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel Jijini Dar es Salaam ikiwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo wenye ushirikiano na Ujerumani.Hapa Baba Askofu Dkt. Mbilu alialikwa kwa  mwaliko maalumu  kutokana na uhusiano mkubwa uliopo na wa muda mrefu  kati ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  na Ujerumani.

 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki amewashukuru washarika wa Usharika wa Tamota na wanadayosisi kwa ujumla kwa namna wanavyoendelea kushikamana na kujitoa katika kumtumikia Mungu.

MATUKIO KATIKA PICHA . Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,Tarehe: 26/10/2023, akiwa katika ziara ya kikazi katika Jimbo la Magharibi, Usharika wa Gombero, ambapo kumefanyika Ibada zilizoambatana na matendo mbalimbali.