ELCT North Eastern Diocese
Katibu Mkuu wa KKKT Mhandisi Robert Kitundu awataka Wakristo kuliombea Kanisa
- Details
Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Mhandisi Robert Kitundu amewataka Wakristo wa KKKT kuendelea kuliombea Kanisa na kulisogeza mikononi mwa Mungu ili liendelee kudumu katika Umoja na upendo wa kweli.
Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo leo tarehe 09/07/2023 kwenye Ibada ya Jumapili iliyofanyika KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani Jimbo la Magharibi Usharika wa Kimara ambapo pamoja na kuliombea Kanisa amewasihi Wakristo kutunza Ulutheri katika kumtukuza Mungu.
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt.Msafiri Joseph Mbilu ambaye yupo katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi anayoifanya KKKT-DMP ni mmoja wa walio shiriki katika Ibada hii.
Mchana wa leo Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu atakuwa na mkutano na Wakristo wote wanaotokea KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Lushoto, Tanga pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo waishio Dar es Salaam kuanzia saa 9:00 Alasiri. Mkutano huu utafanyika kwenye ukumbi wa mikutano KKKT - Mbezi Beach.
- Hits: 1834
Dean Michael Kanju akabidhi pikipiki kwa Chuo cha Biblia Vuga.
- Details
Msaidizi wa Askofu wa KKKT-DKMs Mch Michael Kanju (Kushoto) akimakabidhi Mkuu wa Chuo cha Biblia Vuga Mch. Benson Kimweri Kivuli cha kadi ya Pikipiki
Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju amekabidhi pikipiki 1 kwa Mkuu wa Chuo cha Biblia Vuga Mch. Benson Solomon Kimweri, ikiwa ni hatua za awali za kutatua changamoto ya usafiri Chuo hapo huku akiagiza pikipiki hiyo kwenda kutumika kwa malengo mahsusi yaliyokusudiwa,
Mzaidizi huyo wa Askofu Mch. Michael Kanju amekabidhi pikipiki hiyo kwa niaba ya Baba Askofu Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 04/07/2023 katika Makao Makuu ya KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Lushoto Tanga.
Hii ni kufuatia ahadi ya Askofu Dkt. Msafiri Mbilu aliyoitoa mnamo tarehe 28/06/2023 akiwa katika ziara yake ya kikazi kutoa pikipiki kwa ajili ya Chuo hicho cha Biblia Vuga ambapo pia aliueleza uongozi wa Chuo hicho kuwa mipango ya upatikanaji wa gari kwaajili ya Chuo hicho bado inaendelea.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Mch. Benson Kimweri ameushukuru uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa kuwapatia pikipiki hiyo itakayokuwa msaada katika mambo ya usafiri.
- Hits: 1837
Ungana nasi kuchangia Deni la Dayosisi
- Details
Katika kuungana kwa pamoja kuchangia DENI linaloikabili KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ili kunusuru mali zake zisipigwe mnada sasa unaweza kutumia namba hizi za simu kutoka mitandao ya Airtel Vodacom na Tigo kutuma mchango wako.
- Hits: 1629
Page 4 of 91