ELCT North Eastern Diocese
Askofu Dkt. Mbilu kila Makristo anaowajibu wa Kushuhudia Nuru na Upendo wa Kweli wa Yesu Kristo
- Details
MAKAYO KOROGWE: Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) amewataka Wakristo kuacha kufuata mafundisho potofu na badala yake wachukue jukumu la kuyashuhudia Maandiko Matakatifu kwa wengine.

Akizungumza Alhamisi, Julai 31, 2025, wakati wa Ibada ya Kipaimara iliyofanyika katika Jimbo la Magharibi, Usharika Mteule wa Msomera, Mtaa wa Makayo, Askofu Dkt. Mbilu alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila mmoja kushuhudia nuru ya kweli na upendo wa Yesu Kristo.

Askofu Dkt. Mbilu amewataka washarika wa Mtaa wa Makayo, ambao wengi wao ni jamii ya wafugaji wa Kimasai, kuacha kuwasikiliza watu wanaokwenda maeneo yao na kudai kuleta "nuru ya Wamasai," akisisitiza kuwa Yesu anatosha na yeye ndiye Nuru ya Ulimwengu. Aliwahimiza kuiga mfano wa Yesu Kristo, ambaye aliupenda ulimwengu wote na hakuja kwa ajili ya Wamasai pekee bali kwa ajili ya ulimwengu mzima.
Katika Ibada hiyo ilitanguliwa na ufunguzi wa Kanisa la Usharika Mteule wa Msomera, Mtaa wa Makayo. Jumla ya vijana 64 walibarikiwa na walichangia Tsh. 310,000 na mara baada ya kuungwa mkono na wanaume na wanawake waliohudhuria Ibada hiyo, jumla ya shilingi 585,000 zilipatikana na zitaelekezwa katika ulipaji wa deni la Dayosisi.
Tufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii
- Hits: 5013
Tangazo la nafasi ya kazi Irente Farm
- Details

KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA
DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI
S.L.P 10, (SIMU 027-266002 / Fax 027-2660092), LUSHOTO.
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
TANGAZO LA KAZI NAFASI YA BWANA SHAMBA KITUO CHA IRENTE FARM
Irente Farm ni kituo cha kilimo kinachomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT–DKMs), kilichopo Lushoto, Mkoani Tanga. Kituo hiki ni sehemu ya huduma za maendeleo ya jamii zinazotekelezwa na Dayosisi kupitia miradi ya kilimo endelevu. Katika kuimarisha ufanisi wake, kituo kinatangaza nafasi ya kazi kwa cheo cha Bwana Shamba. Tunakaribisha maombi kutoka kwa watu wenye sifa, uwezo, na maadili mema ya Kikristo kushiriki katika huduma hii muhimu.
Majukumu ya Msingi:
- Kusimamia shughuli zote za kilimo katika shamba la Irente.
- Kupanga, kuratibu na kufuatilia shughuli za uzalishaji wa mazao na ufugaji.
- Kusimamia matumizi bora ya rasilimali za shamba (wafanyakazi, vifaa, mbegu, mbolea n.k).
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu mbinu bora za kilimo na ufugaji.
- Kuandaa ripoti za maendeleo ya kilimo kwa uongozi wa Irente Farm.
- Kushirikiana na taasisi na wadau mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya kilimo.
Sifa za Mwombaji:
- Awe na shahada (degree) katika Kilimo au fani zinazohusiana, kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.
- Awe na uzoefu wa angalau miaka miwili (2) katika kusimamia shughuli za kilimo na ufugaji.
- Awe na uwezo wa kutumia kompyuta na kuandaa ripoti za kazi.
- Awe tayari kuishi na kufanya kazi Irente – Lushoto.
Namna ya Kutuma Maombi:
Maombi yote yaambatane na:
- Barua ya maombi
- Wasifu binafsi (CV)
- Nakala ya vyeti vya kitaaluma
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa au NIDA
Maombi yote yatumwe kwa:
Katibu Mkuu,
KKKT– Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,
S.L.P 10,
LUSHOTO – TANGA
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Mwisho wa Kutuma Maombi: Tarehe 15 Agosti 2025 (saa 9:59 alasiri)
Kumbuka:
Ni waombaji waliokidhi vigezo watakaoitwa kwenye usaili. Kanisa linahimiza usawa wa kijinsia – Wanawake pia wanahamasishwa kuomba nafasi hii.
- Hits: 4325
Page 5 of 134



