ELCT North Eastern Diocese
KKKT-DKMs na maboresho ya Hospitali ya Kilutheri Bumbuli
- Details

KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, inayomiliki Hospitali ya Kilutheri Bumbuli (Bumbuli Lutheran Hospital) imeendelea kufanya maboresho katika Hospitali hiyo baada ya hivi karibuni kutoa mashine ya usingizi (Anesthesia Machine) pamoja na vifaa tiba vingine vya kisasa ambavyo vitasaidia kuendelea kuboresha huduma ya Afya Hospitalini hapo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mwl. Afizai Elisa Vuliva, wakati akikabidhi mashine hiyo kwa uongozi wa Hospitali ya Bumbuli huku akiwataka kutunza mashine hiyo pamoja na vifaa vingine vilivyo pelekwa hospitalini hapo kutoka kwa Shirika la GIZ.
- Hits: 5632
Askofu Dkt. Msafiri Mbilu, Ziarani Nchini Ujerumani
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu yupo katika ziara ya kikazi Nchini Ujerumani ambapo ameambatana na Dean Mteule Frank Mtangi pia wamepata wasaa wa kutembelea Jimbo la Staaken kwenye Jiji la Berlin.
- Hits: 5865
Askofu Dkt. Mbilu, kuhusu zoezi linaloendelea la kuchukuwa maoni juu ya Katiba Mpya ya KKKT
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs), Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Halmashauri ya Katiba ya KKKT, juu ya zoezi linaloendelea la kuchukuwa maoni juu ya Katiba Mpya ya KKKT na kusema kuwa anaamini Katika Mpya ya KKKT, itakuwa jumuishi na italeta umoja wa kweli katika Kanisa.

- Hits: 7203
Page 8 of 134


