ELCT North Eastern Diocese
Kiongozi wa mbio za Mwenge 2023 aridhishwa na ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Lushoto.
- Details
Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto imeupokea Mwenge wa uhuru leo tarehe 14/06/2023 ukiongozwa na kiongozi wa mbio za Mwenge 2023, Ndg Abdalla Shaib Kaim huku akikagua na kufungua miradi mbalimbali.
Ndugu Abdalla Shaib Kaim aliridhishwa na ujenzi wa choo cha matundu sita kinachojengwa katika Shule ya Msingi Lushoto, ambapo mara baada ya kukagua nyaraka za ujenzi huo aliridhia kuweka jiwe la Msingi.
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt Msafiri Joseph Mbilu alikua miongoni mwa viongozi wa Wilaya ya Lushoto katika kupokea mwenge huo na alipata wasaa wa kufanya maombi na kutoa baraka zake kwa viongozi hao wa Mwenge.
Askofu Dkt. Msafiri Mbilu akisalimiana na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndg. Abdalla Shaib Kaim.
Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akifanya maombi na viongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023.
Sehemu ya faida za Mwenge wa Uhuru Kitaifa na Kimataifa ni pamoja na kuendelea kuhamasisha ari ya wananchi kujitegemea na kuwekeza katika maeneo mbalimbali katika Taifa letu. Kauli Mbiu katika Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2023 ni “Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa.”
- Hits: 2468
Safari ya mwisho ya Mzee Karata mwili wali wake waziku Old Korogwe-Tanga
- Details
PICHA ZA MATUKIO mbalimbali ya Ibada ya Mazishi ya Marehemu Mzee Moses Gao Karata, yaliyofanyika leo tarehe 13/06/2023 katika Jimbo la Tambarare Usharika wa Mtonga, Ibada imeongozwa na Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Kanju akishirikiana na Mkuu wa Jimbo la Tambarare, Mch Frank Mtangi.
- Hits: 1807
TANZIA- Baba Mzazi wa Mchungaji William Karata wa Usharika wa Mtonga amefariki dunia
- Details

- Hits: 1833
Matukio katika picha.
- Details

- Hits: 1701
Page 6 of 91