ELCT North Eastern Diocese
Marafiki wa Jimbo la Tambarare Vlotho Ujerumani wakutana na Askofu Dkt.Mbilu.
- Details

Mwendelezo wa Ziara ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, tarehe 08/03/2024 amefanya ziara katika Jimbo la Vlotho nchini Ujerumani lenye urafiki na Jimbo la Tambarare la KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. KATIKA PICHA, ni miongoni mwa Wajumbe wa Kamati ya Uhusiano chini ya Mwenyekiti wao Mch. Markus Freitag.(wa kwanza kutoka kulia).

Mwenyekiti wa Undugu kati ya Jimbo Vlotho nchini Ujerumani na KKKT-DKMs Jimbo la Tambarare ,Mch. Markus Freitag (wa kwanza kutoka kushoto), mwenzi wa Askofu Dkt. Mbilu Mwl. Marry Jally (wa pili kutoka Kushoto), Askofu Dkt. Msafiri Mbilu (wa tatu kutoka Kushoto) pamoja na mwezi Mwenyekiti wa Undugu Mch. Markus Freitag, (wa nne kutoka Kushoto).
- Hits: 9253
Mkuu wa Kurugenzi ya Uhusiano wa Kimataifa kutoka Ujerumani kuitembelea KKKT-DKMs mwezi Julai 2024.
- Details

- Hits: 9347
Mwendelezo wa ziara ya Askofu Dkt. Msafiri Mbilu nchini Ujerumani.
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ambaye yupo ziarani nchini Ujerumani anaendelea na ziara yake na leo tarehe 05/03/2024 amekutana na kufanya mazungumzo na marafiki wa Dayosisi yetu. Katika picha ni sehemu ya watumishi mbalimbali waliowahi kufanya kazi kwenye Hospitali ya Wagonjwa wa akili ya Lutindi Mental Hospital, inayomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
- Hits: 9157
Askofu Dkt. Mbilu ziarani nchini Ujerumani
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, yupo ziarani nchini Ujerumani, ambapo akiwa nchini humo atashiriki Ibada ya kumuaga Katibu Mkuu wa chama Cha kiinjili Cha kimisioni (UEM) anayemaliza muda wake Mch.Volker Dally na kuingizwa kazini kwa Katibu Mkuu mpya wa UEM Mch. Dkt. Andar Parlindungan,ambaye awali alikuwa Katibu mtendaji wa idaraya mafunzona uwezeshajiwa UEM.Ibada itafanyika tarehe 01/03/2024 
- Hits: 9115
Page 34 of 137

