ELCT North Eastern Diocese
Waziri Ofisi ya Rais Uwekezaji na Mipango awahimiza Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCT kujikita katika uwekezaji
- Details
Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo inajulikana kwa kifupi kama CCT (Christian Council of Tanzania), ni Taasisi ya Ki-ekumene inayowakilisha Umoja wa Madhehebu ya Kikristo ya Kiprotestanti. Kwa sasa CCT inaundwa na Makanisa mbalimbali Wanachama na Vyama vya Kikristo au vyenye mwelekeo wa kikanisa kutoka Tanzania Bara na Visiwani. Taasisi hii ilianzishwa rasmi tarehe 23 Januari, 1934 kutokana na maono ya Wamisionari kutoka Kanisa Anglikana, Kanisa la Moravian na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri. Wamisionari hawa walipata maono ya kujenga umoja kati ya makanisa wanachama ambao utajihusisha na masuala mbalimbali ya ki-imani, kimaendeleo na kijamii. Muungano huu ulijulikana kwa jina la Kiingereza, Tanganyika Missionary Council (TMC).
Mnamo mwaka 1964 Mungu aliwapa maono watumishi wake Baba Askofu Stephano Reuben Moshi (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania), Baba Askofu Theofilo Kisanji (Kanisa la Moravian Tanzania) na Baba Askofu Mkuu John Sepeku (Kanisa Anglikana Tanzania) kubadilisha usajili wa TMC kuwa Christian Council of Tanzania (CCT), jina linalotumika hadi sasa. Idadi ya Makanisa yaliyopo chini ya CCT imekuwa ikiongezeka kutoka Makanisa matatu (3) ya mwanzo mwaka 1934 hadi kufikia makanisa ya Kiprotestanti kumi na mbili (12) yaliyopo mwaka 2021.
Kwa sehemu kubwa Makanisa Wanachama wa CCT yanafuata mapokeo ya Makanisa ya Kiinjili. Aidha, ili kuwezesha kukua na kuimarika kwa umoja wa kweli, Makanisa Wanachama yanatumia utaratibu unaofanana katika mambo muhimu. Mambo hayo ni pamoja na Ukiri wa Imani ya Mitume (Apostles Creed), Ukiri wa Imani ya Nikea (Nicene Creed) katika kuendeleza ufalme wa Mungu kwa njia ya mahubiri na kuunganishwa kuwa mwili mmoja katika Yesu Kristo.
- Hits: 2525
Askofu Dkt. Mbilu aongoza Ibada ya Kustaafu kwa Heshima kwa Mchungaji Shemkala
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 30/06/2024 ameongoza Ibada ya Kustaaafu kwa heshima kwa Mch. Lewis Fredrick Shemkala hii ikiwa ni kwa mujibu wa Katiba ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mchungaji Lewis Fredrick Shemkala, amefikia umri wa kustaafu baada ya kuitumikia Dayosisi hii kwa miaka 33 ya Uchungaji na miaka 2 ya Uinjilisti.
- Hits: 2703
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Mlalo , Youths Confirmation at Mlalo Lutheran Parish.23/06/2024
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewashukuru Washarikwa wa Usharika wa Mlalo na wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa namna wanavyojitoa katika kumtumikia Mungu.
- Hits: 2464
Ziara ya Baba Askofu Dkt. Mbilu katika Taasisi ya Elimu ya Kolowa Technical Training Institute (KOTETI)
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ameupongeza uongozi wa Taasisi ya Elimu ya Kolowa Technical Training Institute (KOTETI), kwa kazi nzuri inayofanyika katika nyanja ya mafunzo kwa kuzingatia kasi na viwango katika utoaji wa Elimu katika taasisi hiyo inayomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
- Hits: 2420
Page 11 of 122