Njooni tumwimbie BWANA wimbo mpya, Safina Lutheran Choir ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Jimbo la Pwani Usharika wa Pongwe wameandaa tamasha la Uimbaji,
wanapenda kukualika  kushiriki katika tamasha  litakalo fanyika Jumapili ya tarehe 05/12/2021  kuanzia Saa 7:00 Mchana. Katika Usharika wa Pongwe.

 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 30/11/2021 amehitimisha ziara yake ya siku mbili katika Usharika wa Pongwe, Jimbo la Pwani.

Baba Askofu Dkt. Mbilu amehitimisha ziara yake hiyo leo kwa kuongoza Ibada ya uwekwaji wa jiwe la msingi la Kanisa katika Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Machemba pamoja na ufunguzi wa Kanisa katika Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Kilapula.

Katika Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Machemba, Baba Askofu ametoa kiasi cha Tsh 100,000 kuunga mkono kazi ya Bwana inayoendelea katika Mtaa huo,kwa upande mwingine Eng. Benedict Lema ametoa kiasi cha Tsh 2,000,000 milioni mbili kwaajili ya ujenzi wa Kanisa hilo unaoendelea.

MKUU WA JIMBO LA PWANI, MCH. THADEUS A. KETTO

Msafara wa Baba Askofu chini ya Mkuu wa Jimbo la Pwani Mch. Thadeus A. Ketto wameahidi kutoa kiasi cha Tsh. 1,150,000 zitakazo tumika katika ujenzi huo wa Kanisa unaoendelea.

Hata hivyo mara baada ya Ibada katika Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Machemba, Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alijumuika na washarika wa Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Kilapula kwenye Ibada ya Shukrani ya ufunguzi wa Kanisa.Baba Askofu amewapongeza washarika wa mtaa huwa wa Kilapula kwa ujenzi mzuri wa  nyumba hiyo ya Ibada kwani imejengwa katika kiwango kizuri na litadumu kwa kipindi kirefu.

 

Mtaa wa Kilapula ulianzishwa tarehe 20/08/2008 ukiwa chini ya Mtaa wa Kilole uliokua katika Usharika wa Kana chini ya Mch. Lewis Shemkala na Mitaa hii ilitunzwa na Mwj Hemba.

Washarika wa Mtaa wa Kilapula hawajkusita kutoa  shurani zao za pekee kwa watumishi waliowatunza kiroho katika ujenzi huo wa Kanisa.

  • Mch. Lewis Shemkala Mtaa huo ulipokuwa chini ya Usharika wa Kana na yeye aliwezesha upatikanaji  wa eneo hilo.
  • Mch Neema Kamendo
  • Mch Dkt Msafiri Mbilu
  • Mch.Thadeus A. Ketto.

Hadi leo hii Mtaa huo wa Kilapula una jumla ya Wakristo 201, watu wazima ME. 52, KE 75 JUMLA = 127, na Watoto ME 32 KE 42 JUMLA 74.Ikumbukwe hapo jana Baba Askofu Dkt. Mbilu aliongoza Ibada ya ufunguzi wa darasa la Watoto wa Shule ya Jumapili,katika Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Saruji.na ujenzi wa Darasa hilo ulianza  mwezi June,2021 chini ya Mch. Nkanileka Chedi.

 Kwa upande mwingine Baba Askofu amepongeza vikundi vya kwaya vya Usharika wa Pongwe na Mitaa yake kwa ujumla kwa uimbaji mzuri upigwaji wa vyombo vya muziki (LIVE) kwani hiyo ndio maana ya kumwimbia Mungu wimbo mpya kila siku.

Hakusita kukemea uimbaji wa kutumia flash yaani matumizi ya nyimbo zilizo rekodiwa tayari kwani njia hiyo inadumaza uimbaji, walimu wa muziki wamekumbushwa kutunga nyimbo nzuri zenye maneno mazuri na zinazoendana na nyakati.

 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,amewapongeza washarika wa Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Saruji kwa moyo wakujitoa  katika kumtumikia Mungu.

 

Pongezi hizo amezitoa leo tarehe 29/11/2021 kwenye Ibada ya uwekwaji wa jiwe la msingi na ufunguzi wa darasa la Watoto wa shule ya Jumapili, mahali ambapo Watoto hao wataabudia.

Leo tarehe 28/11/2021 ni siku ya Bwana ya kwanza katika maajilio, advent ya kwanza.kila mwaka wanawake wanapata nafasi ya kuongoza Ibada na kufanya maombi na maombezi kwa ajili ya familia,Sharika,Majimbo na Dayosisi kwa ujumla.Sharika zote za KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki zimeungana katika maombi hayo.

Katika Ibada  iliyoongozwa na wanawake, Kanisa Kuu Lushoto wametambua umuhimu wa mfuko wa maendeleo na kumuomba Mungu malengo na maono ya viongozi wa Dayosisi yapate kutimia kupitia mfuko huo.

Ibada hiyo iliyo ongozwa na  wanawake katika Kanisa Kuu Lushoto imeongozwa na Mwinjilisti Esther Mahimbo, na Mwenyekiti wa wenzi wa wachungaji kutoka KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Janeth Kalinga ndiye aliye hubiri neno la Mungu kutoka kitabu cha Mathayo 24:42-44.

Kwa upande mwingine Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt Msafiri Joseph Mbilu amewashukuru UEM kwa kuratibisha na kuwezesha warsha iliyo unganisha kundi kubwa na lililokamili la wake wa wachungaji na mashemasi kutoka KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki pamoja na KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani,katika warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano SEKOMU.

Askofu Dkt. Msafiri Mbilu pia amewashukuru wake wa wachungaji kutoka Dayosisi ya Mashariki na Pwani kwa kutoa kiasi cha Tsh 500,000 (Mbegu) ili wake wa wachungaji na mashemasi waanzishe kikundi cha Vicoba ambacho, Baba Askofu ameahidi uongozi utasimamia kikundi hicho.

Mbali na kiasi hicho walicho kitoa wameweka alama ya kuimarisha undugu kati ya Dayosisi hizi mbili, katika vituo vya Dayosisi kama ifuatavyo.Shule ya Watoto wenye ulemavu wa akili Irente Tsh. 500,000, Kituo cha mafunzo na malezi bora kwa Watoto yatima Irente Tsh.500,000 pamoja na Tsh 500,000 kwaajili ya Shule ya wasioona Irente.